

Lugha Nyingine
保时捷中国总裁陷桃色传闻 新高管去年在德吃了败仗
BEIJING- Rais wa China Xi Jinping amempongeza Jennifer Simons kwa kuchaguliwa kuwa rais wa Suriname, na katika salamu zake za pongezi zilitozumwa Ijumaa, Rais Xi ameielezea Suriname ni mshirika wa China katika ushirikiano wa kimkakati katika eneo la Karibiani.
"Shukrani kwa juhudi za pamoja za pande zote mbili, uhusiano kati ya China na Suriname umefurahia ukuaji mzuri kwa hatua madhubuti, ushirikiano wa kufuata hali halisi umefanyika katika sekta mbalimbali na kupata matokeo yenye ufanisi mkubwa, na pande hizo zimefanya uratibu wa karibu katika mambo ya pande nyingi katika miaka 49 iliyopita tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia” Rais Xi amesema.
Amesema, anaweka umuhimu mkubwa sana kwenye ukuaji wa uhusiano kati ya China na Suriname na anapenda kushirikiana na rais mteule Simons katika kuzidisha ushirikiano wa kirafiki wa kunufaishana na kukuza zaidi ushirikiano wa kimkakati wa pande mbili ili kuleta manufaa zaidi kwa watu wa nchi hizo mbili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma