

Lugha Nyingine
韩国举办机器人滑雪赛 英媒:可媲美平昌冬奥会
Habarini! Mimi ni Sisi, mpenda kusafiri! Leo ni siku ya kuanza kwa kipindi cha Joto Kubwa, au Dashu katika vipindi 24 vya hali ya hewa katika Kalenda ya kilimo ya China, kilele cha majira ya joto zaidi na kipindi cha mwisho kwa majira ya joto. Hivi sasa, niko Turpan, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, kaskazini-magharibi mwa China, unaojulikana kama "Ardhi Inayowaka" ya China. Hebu tujionee pamoja ukali wa kweli wa majira ya joto!
Kwa wakulima kote China, Joto Kubwa ni kipindi muhimu cha kukimbiana na wakati kwa ajili ya kuvuna mpunga wa msimu wa mapema na kupanda mazao yanayofuata. Inaonyesha hekima ya ustaarabu wa kale wa kilimo wa China, ulioboreshwa kwa kuishi kwa mapatano na mwenendo wa mazingira ya asili kwa zaidi ya milenia.
Hapa Turpan, halijoto katika Milima Moto inaweza kuzidi nyuzi joto 70 Celsius (nyuzijoto 158 Fahrenheit). Hata hivyo, katika joto hili kali la kutoa watu jasho, utamu hustawi. Katika Bonde la Zabibu, hewa imejaa harufu nzuri ya zabibu zilizoiva kama vito vya kijani chini ya viambaza vya fito. Utamu huu unatokana na uvumbuzi wa ajabu zaidi ya miaka 2,000 iliyopita- mfumo wa kisima cha Karez. Mifereji hii ya chini ya ardhi hupeleka maji kwa ukimya kupita udongo wa changarawe ili kumwagilia bustani kubwa, ikionyesha falsafa ya ikolojia ya China kuhusu mapatano kati ya binadamu na mazingira ya asili.
Sehemu mbalimbali duniani, watu wana njia zao za kukabiliana na joto. Nchini Japan, joto la majira huo hugongana na "Doyo no Ushi no Hi," wakati watu wanapofurahia eel iliyochomwa ili kurejesha nguvu zao. Nchini Korea Kusini, watu huongeza nguvu zao kwa bakuli la supu ya kuku ya ginseng wakati wa siku za joto zaidi. Nchini Thailand, tamasha la Khao Phansa huingia msimu wa mvua, wakati mishumaa inapowashwa na kuelea hadi mahekalu—ikitoa wakati mzuri wa utulivu na ibada za matambiko katikati ya mwako wa majira ya joto.
"Ni lini jua hili kali la kuchoma mwili litapita? Hakuna upepo unaoonekana." Kikiwa ni kipindi cha mwisho cha majira ya joto, Joto Kubwa ni alama ya hali ya juu ya mazingira ya asili na mwangwi wa maisha. Ni kwa namna gani, unalishinda joto la majira ya joto? Je! una vidokezo vyako mwenyewe vya kupoza joto au kumbukumbu pendwa za msimu huo?
Tuambie simulizi yako!
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma